Klabu ya Manchester United imeshindwa kupata matokeo katika uwanja wake nyumbani leo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Newcastle United.
Man United wanapata suluhu ya kwanza msimu katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kuopoteza michezi mitatu na kushinda mitano huku wakibaki nafasi ya tano kwa alama 16 huku Newcastle wao wakisalia nafasi ya sita na alama zao 15 baada ya kuchezxa michezo tisa kila mmoja.
Klabu ya Manchester United ambayo ilianza msimu vibaya kwa kupoteza michezo miwili mfululizo huku wakirejea na kushinda michezo minne mfululizo kabla ya kuja kupoteza kwa iabu dhdi ya mahasimu wao klabu ya Manchester City.
Mpaka sasa klabu ya Manchester United inaonekana bado haijatulia kutokana na matokeo ambayo inakua ikiyapata chini ya mwalimu mpya Eric Ten Haag ambaye amejiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea Ajax.
Jambo ambalo pia linaonekana kuwakwamisha Manchester United ni kutokua na muendelezo wa viwango bora kwa wachezaji wake ambao mara nyingi wanacheza vizuri michezo kadhaa na kucheza vibaya michezo mingine.

