Klabu ya soka ya Geita Gold imefanikiwa kuifunga klabu ya Ihefu Fc kutoka jijini Mbeya kwa goli moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Nyankumbu mkoani Geita.
Bao pekee la Juma Luizio liliweza kuwapata wenyeji alama tatu muhimu kwenye mchezo na kuwaacha klabu ya Ihefu ikiwa imetepeta kushika mkia katika msimamo wa ligi kuu ya NBC huku Geita wao wakitakata.
Klabu ya Geita Gold imefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kuifunga Ihefu na kufikisha alama 21 na kuishusha Singida Big Stars waliokua nafasi ya nne kwenye msimamo.
Kiungo wa klabu hiyo Saido Ntibazonkiza pia aliendelea kutakata leo baada ya kupiga pasi ya bao kwenda kwa mfungaji wa pekee wa bao Juma Luizio mpaka sasa mchezaji huyo kahusika kwenye mabao nane akifunga mabao matatu na kupika matano.

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

