Uongozi wa Pan African umefunguka kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanazipata pointi tatu katika kila mchezo wa Championship ili kutimiza malengo yao.

Tangu Iddy Cheche aichukue timu hiyo kama Kocha Mkuu, kikosi hicho kimefanya vizuri kwenye ligi ya Championship.
Jana Pan African ilimenyana na Biashara United kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau alisema “Tunamshukuru Mungu tumeibuka na ushindi huu ambao ulikuwa ni mipango yetu.

“Kila mchezo kwetu ni fainali hivyo mipango tuliyonayo kwa sasa ni kupata pointi tatu kwenye kila mchezo ili kuhakikisha tunatimiza malengo ya kurudisha heshima ya klabu yetu.
“Wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili hivyo watarejea mazoezini jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KenGold ya Mbeya.”
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.


