Kikosi cha Pan African kesho jumatano kinatarajia kuondoka kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Copco.

Pan inayonolewa na Kocha Mkuu, Iddy Cheche kinacheza mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate.

Pan African, Pan African Kuifuata Copco Kesho, Meridianbet

Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema: “Kikosi chetu kipo vizuri na tayari leo jumanne kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi.

“Kuna mchezaji ambaye ni Ayoub Mohamed alikuwa majeruhi tayari ameanza mazoezi na hivi karibuni ataonekana tena kwenye kikosi.

“Timu itaondoka Dar kesho jumatano ili alhamis wafike Mwanza na kupumzika, Ijumaa watafanya mazoezi mepesi tayari kwa mchezo wa jumamosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa