Uongozi wa Azam FC umefunguka kuwa haufikirii ubingwa wa ligi kuu licha ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Azam leo watashuka katika dimba la Azam Complex kuchuana na Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wao wa 12 tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.

AZAM, Azam Hawafikirii Ubingwa Ligi Kuu, Meridianbet

Kikosi hicho kinachonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala kimefanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kukudanya pointi…

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea katika mchezo wa leo, Kocha Kali alisema wao wanahitaji kushinda kila mchezo uliopo mbele yao kwa ajili ya kutimiza malengo.

“Timu ipo vizuri kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting, wachezaji wana morali na tunawakaribisha mashabiki wetu uwanjani ili kuwapa sapoti vijana.

“Mipango yetu ni kupata ushindi, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tunaenda kupambana tuweze kupata ushindi ili mipango yetu itimie.

“Sisi hatufikirii ubingwa kwa sasa bali tunafikiria kupata ushindi katika kila mchezo uliopo mbele yetu kwani hilo litaamua ubingwa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa