Kikosi cha Yanga kimerejea kambini leo jumanne kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Novemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Nabi, Nabi Arejesha Nyota Wake Kambini, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema: “Baada ya kurejea Dar kutokea Mwanza kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar wachezaji walipewa mapumziko.

“Tangu tuondoke kwenda Tunisia wachezaji wetu hawakupata muda wa kupumzika hivyo benchi limetoa mapumziko mafupi.

“Leo asubuhi wachezaji walianza kuripoti kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Singida Big Stars.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa