Beki wa kimataifa wa Brazil Marquinhos amefungaka na kusema timu hiyo iko vizuri hata ikimkosa mshambuliaji wao Neymar Jr ambae alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Serbia.
Neymar atakosekana kwenye michezo iliobakia ya makundi baada ya kuumia enka katika mchezo ambao Brazil ilishinda kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya taifa ya Serbia siku ya alhamisi.
Marquinhos anaeleza wangetamani kua na Neymar kwenye kikosi kwasababu ni jambo zuri kuona wachezaji wote 26 wako imara lakini wanajiamini kwa asilimia 100 bila ya Neymar wanaweza kufanya vizuri katika michezo iliyobakia.
Marquinhos pia aliongeza baada ya kuulizwa kuhusu majeraha ya Neymar na kusema “Alijiskia vibaya kwakua amekua akiota kila siku kuhusu hii michuano,Lakini kwasasa yupo kwenye majeraha kama wachezaji tunaelewa anapitia wakati gani na tunamtakia kila la kheri aweze kurejea mapema”
Brazil watacheza mchezo wao wa pili katika kundi dhidi ya Uswisi hapo kesho na kama watafanikiwa kupata ushindi kimahesabu watakua wametangulia kwenye hatua ya 16 kwenye kundi hilo.

