Martinez: Kupoteza dhidi ya Saudi Kumetujenga

Beki wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester United Lisandro Martinez anaamini kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Saudia Arabia kumewaimarisha na kuwajenga kuelekea michezo mingine.

Timu ya taifa ya Argentina ilipoteza mchezo wake wa ufunguzi kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Saudia jambo lililowashtua watu wengi ukiachana na timu hiyo, Hivo beki huyo anaamini baada ya mchezo ule waliimarika kwa kiwango fulani kwani walipata matokeo mazuri dhidi ya Mexico.martinezLisandro Martinez anasema anaamini kupoteza mchezo unakufanya kujifunza vitu ambavyo huwezi kujifunza wakati unapata matokeo mazuri au kupata mafaniko.beki anasema baada ya kupoteza inawafanya kujiandaa vizuri zaidi ili kuweza kupata matokeo mazuri siku nyingine.

Timu ya taifa ya Argentina wanatarakia kucheza mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Poland hapo kesho mchezo ambao unawahitaji Argentina kushinda ili kufuzu au kupata sare pia huku ikitegemea na mechi kati ya Saudia Arabia dhidi ya Mexico.martinezBeki Martinez pia amewaasa wenzake wanaenda kucheza na mpinzani mgumu ambae ni Poland ambao wana mshambuliaji mzuri Roberto Lewandowski, Huku akimsifu mshambuliaji huyo akidai ni mtu wa kuchungwa zaidi kwenye mchezo kwani mtu mwenye uwezo mkubwa ambae anaweza kuwaletea madhara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.