Timu ya taifa ya Senegal pamoja na Uholanzi wamefuzu hatua ya 16 kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kushinda michezo yao ya mwisho ya kundi hilo jioni ya leo.
Senegal ambao walifungwa mechi yao ya kwanza dhidi ya Uholanzi ila walisawazisha makosa yao na kuweza kushinda michezo yao miwili iliyofuata katika kundi hilo na kuwafanya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo tangu 2002.
Senegal wamefanikiwa kuifunga Ecuador mabao mawili kwa moja leo huku magoli ya Ismaila Sarr pamoja na nahodha wa timu hiyo Kalidou Coulibaly yaliiwezesha Simba wa Teranga kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo huku bao la kufutia machozi la Ecuador likifungwa na kiungo Moises Caicedo.
Timu ya taifa ya Uholanzi wao wakiendeleza rekodi yao ya kutokutolewa kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuwapiga wenyeji Qatar mabao mawili kwa bila. Mabao ya Coady Gapko pamoja na Frenkie De Jong yalitosha kuipelekea Uholanzi hatua ya 16 bora ya michuano hiyo wakiwa na alama zao saba kama vinara wa kundi A.
Kinda wa timu hiyo Coady Gapko ameendelea kuonesha makali yake baada ya kufunga lake la tatu kwenye michauno hiyo, Baada ya kufunga katika mchezo wa leo na kuweka rekodi ya kufunga katika mchezo wa michuano hiyo kwenye hatua ya makundi.

