Conte: Tutaingia Sokoni January ila Kwa Kuangalia Malengo ya Klabu

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amezungumza kuhusu klabu hiyo kuingia sokoni kwenye dirisha la usajili mwezi Januari.

Kocha huyo amezungumza baada ya kutoka suluhu katika mchezo dhidi ya klabu ya Brentford ameweka wazi kua klabu hiyo itaingia sokoni kwenye dirisha la usajili mwezi Januari, Lakini watazingatia matakwa ya klabu hiyo.conteKocha Antonio Conte amesema kuna uwezekano wa klabu hiyo kuingia sokoni, Lakini wataangalia namna gani wanaweza kufata maono ya klabu hiyo ambayo inataka kuwekeza zaidi kwa vijana zaidi.

Klabu ya Tottenham ina mpango zaidi wa kuwekeza kwa vijana wadogo zaidi kama ambavyo kocha huyo amesema na kutoa mifano kwa wachezaji wadogo kama Kulusevski na Rodrigo Bentacur ambao wana umri mdogo na wanapatikana kwa bei nafuu.conteKocha Antonio Conte amesisitiza watatafuta namna ya kuingia sokoni Januari na kutafuta wachezaji wazuri wenye umri mdogo, Lakini wachezaji hao lazima wawe na bei inayoweza kufikiwa na klabu hiyo kutokana malengo waliyojiwekea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.