Coastal Union Yalazimishwa Sare Nyumbani

Klabu ya Coastal Union imelazimishwa sare na klabu ya Namungo Fc kutoka mkoani Lindi ya bao moja kwa moja katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa katika dimba la CCM Mkwakwani Tanga.

Klabu ya Coastal Union inashindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi ya pili mfululizo na hiyo ni baada ya kulazimishwa sare na Namungo Fc wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Klabu hiyo ilipata sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliopita na leo tena wamepata sare katika mchezo dhidi ya Namungo.coastal unionMchezo huo uliokua na kasi na kila timu ikonekana kua na uchu wa kupata matokeo klabu ya Namungo ndio walikua wakwanza kupata bao dakika ya 47 ya mchezo kupitia kwa Ibrahim Abdallah kabla ya Maulid Maabad kuisawazishia Coastal Union dakika ya 60 ya mchezo kupitia mkwaju wa penati.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja jambo ambalo linaendelea kuwadidimiza wagosi wakaya kutoka mkoani Tanga, Kwani wako kwenye nafasi ya 14 wakiwa na alama zao 17 nafasi ambayo sio nzuri.coastal unionMchezo huo ambao uliibuka utata baada ya mwamuzi wa mchezo kuonekana kutoa penati ambayo sio sahihi kw upande wa Coastal Union ambayo ilisababisha klabu hiyo kusawazisha bao, Tukio hilo limezua gumzo kwa kiwango kikubwa na wadau wengi wa mpira wakitaka mwamuzi huyo afungiwe kutokana na maamuzi hayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.