Klabu ya Santos kutokana nchini Brazil imepiga chini mpango wa kutaka kustaafisha jezi namba 10 iliyokua ikivaliwa na gwiji wa duniani klabuni Pele.
Gwiji Pele ambaye ameripotiwa kufariki mwanzoni mwa wiki hii huko Brazil klabu ya Santos ndio klabu ambayo ameitumikia kwa kipindi kirefu cha maisha yake ya soka kwa uwezo mkubwa, Hivo kulikua na taarifa kua klabu hiyo ingestaafisha jezi namba 10 iliyokua ikivaliwa na gwiji huyo.
Kulitokea pande mbili baada ya wazo la kustaafisha jezi hiyo namba 10 kuletwa mezani na rais wa klabu ya Santos, Kwani kuna upande uliunga mkono wazo hilo lakini kuna upande ulikataa na kusema gwiji Pele alifanya mahojiano mwaka 2017 na kusema jezi yake isistaafishwe na iendelee kutumika.
Gwiji huyo ambaye ni mwanadamu pekee aliefanikiwa kushinda mataji mattau ya kombe la dunia anapewa heshima kubwa sana klabuni hapo pamoja na dunia nzima kutokana na mambo aliyoyafanya katika mpira wa miguu.
Taarifa kutoka nchini Brazil zilieleza kua mwanae na gwiji huyo aliomba jezi ya baba yake kustaafishwa klabuni hapo baada ya kufariki ili kumuenzi na kumpa heshima, Lakini mpango huo umepigwa chini baada ya video ya gwiji huyo kupatikana akisema mwenyewe kua jezi yake isistaafishwe iendelee kutumika.

