Nyota wa zamani wa vilabu vya Manchester United, Real Madrid,Juventus na Sporting Lisbon Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia amesema kazi yake barani ulaya ameshaimaliza.
Leo kwa mara ya kwanza ya kwanza nyota huyo amezungumza na wanahabari baada ya kutangazwa rasmi kua mchezaji wa klabu ya Al Nassr, Na kupitia mkutano huo wa wanahabari Ronaldo amezungumza mambo tofauti tofauti.
Staa huyo amesema kua sio kwamba vilabu mbalimbali barani ulaya havikumtaka ni kua yeye ameamua kujiunga na klabu ya Al Nassr kwajili ya kupata changamoto mpya katika maisha yake ya mpira, Lakini pia akieleza kazi yake barani ulaya imekwisha kwani amecheza vilabu vikubwa zaidi barani humo.
Staa huyo alisisitiza zaidi kwa kusema amefanikiwa kushinda kila kitu kwenye ngazi ya klabu huko barani ulaya huku akichecheza vilabu vikubwa barani ulaya kama Real Madrid, Manchester United na klabu ya Juventus ambapo alifanikiwa kushinda kila taji aliloshindania akiwa ndani ya vilabu hivo.
Cristiano Ronaldo anakua mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani baada ya kujiunga klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia, Mchezaji huyo pia amesema yeye hajali chochote ambacho watu wanazungumza juu yake baada ya kutimkia Uarabuni kwani wengi wao hawajui mpira na kusema anafurahia maamuzi aliyoyafanya.

