Staa wa zamani wa klabu ya Manchester United, Real Madrid, na Juventus Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Rabia ameendeleza ubabe wake kua mchezaji mwenye ushawishi mkubwa.
Staa huyo ambaye amejiunga na klabu ya Al Nassr siku mbili zilizopita na kufanikiwa kua mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwasasa. Ronaldo ameweza kuendeleza ushawishi wake baada ya kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudia Rabia.
Mwaka 2018 Ronaldo alipojiunga na klabu ya Juventus klabu hiyo ilikua na wafuasi wachache katika mitandao ya kijamii lakini baada ya kujiunga na timu hiyo ilifanikiwa kuongeza idadi kubwa sana ya mashabiki, Vilevile kwa klabu ya Manchester United mwaka 2021 ambapo alifanikiwa kuongeza idadi kubwa ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya Ronaldo kujiunga na klabu ya Al Nassr klabu hiyo ilifanikiwa kuongeza idadi kubwa ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii haswa mtandao wa kijamii wa Instagram, Klabu hiyo ilikua na wafuasi laki nane kwenye mtandao wao wa kijamii wa Instagram ili baada ya kutangazwa kwa staa huyo kujiunga na Al Nassr timu hiyo imefanikiwa kufikisha wafuasi milioni tano na laki tano mpaka sasa.
Ronaldo alipojiunga na Al Nassr ameonesha nguvu yake ya ushawishi kwa mara nyingine tena baada ya kuhama na kijiji chake kama ilivyo kawaida, Staa huyo kwasasa ameondoka rasmi barani ulaya na kuelekea Uarabuni tofauti na ilivyosemekana awali kua anatafuta timu inayocheza ligi ya mabingwa barani ulaya.

