Klabu ya soka ya Arsenal vinara wa ligi kuu ya Uingereza ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la kiungo wa klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine Mykhaylo Mudryk.
Klabu ya Arsenal imekua ikimfatilia kiungo huyo kwa muda mrefu sasa huku dau la mchezaji huyo ndio limekua likiwarudisha nyuma washika mitutu hao wa jiji la London, Lakini taarifa zinaeleza klabu hiyo leo itafanya mazungumzo ya moja kwa moja na klabu ya Shakhtar Donetsk ili kumalizana na klabu hiyo.
Vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wameweka kiasi cha Euro milioni 70 mezani kwajili ya kunasa huduma ya kiungo Mykhaylo Mudryk ambaye ameonesha ubora mkubw ndani ya klabu ya Shakhtar Donetsk. Klabu hiyo inataka kuhakikisha usajili huo unakamilika mapema ili mchezaji huyo aweze kujiunga na klabu hiyo.
Mpaka sasa taarifa zinaeleza kua mchezaji mwenyewe Mykhaylo Mudryk ameonesha nia ya kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal, Huku klabu ya Shakhtar Donetsk wao wakihitaji kuweka sawa masuala ya nyongeza ya dau endapo mchezaji huyo atafanya vizuri zaidi siku za mbeleni.
Klabu ya Arsenal imedhamiria kwa kiwango kikubwa kukiimarisha kikosi chake msimu kwajili ya kuendelea kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza ambapo mpaka sasa wanaongoza ligi. Washika mitutu wa London wamekua kwenye ubora mkubwa kuanzia ligi inaanza mpaka sasa.

