Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameonekana hajali kuhusu ubingwa wa Uingereza tena baada ya kupoteza kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Manchester Derby.
Kocha Guardiola amefanya mazungumzo na wanahabari baada ya mchezo wa Derby dhidi ya klabu ya Manchester United ambao uliisha kwa klabu yake kupoteza alinukiliwa akisema ” Sijali kuhusu kombe la ligi na Carabao, Hatuwezi kushinda, Tulishinda sana hivo si tatizo” Hayo yamekua maneno ya kocha huyo baada ya kupoteza mchezo Derby ya Manchester.
Klabu ya Manchester City sasa ipo nyuma kwa alama tano dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza kjlabu ya Arsenal huku klabu hiyo ikiwa ina mchezo mkononi, Hivo klabu ya Arsenal ikishinda mchezo wake w kesho dhidi ya klabu ya Tottenham itaiacha klabu hiyo kwa alama nane.
Pep Guardiola anaonekana kukata tamaa ya kubeba ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kupata matokeo yasiyordhisha msimu huu katika michezo tofauti tofauti, Na kutokana na kauli yake aliyoitoa leo ni wazi anaiona nafasi ndogo ya klabu yake kuweza kutetea taji la ligi kuu ya Uingereza.
Kocha huyo anasema sio kila siku watashinda wao na kukiri kuhuzunishwa na matokeo ambayo ameyapata katika michezo miwili ya hivi karibuni, Huku yeye akiamini tatizo sio kupoteza mchezo tatizo ni namna ambayo wanapoteza mchezo hii inaonesha wazi kocha Guardiola haridhishwi na namna wanavyocheza vizuri na mwisho wanapoteza mechi kizembe.

