Klabu ya Chelsea imefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya muda mrefu ikifanikiwa kuifunga klabu ya Crystal Palace goli moja kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge.
Klabu ya Chelsea ambayo ilicheza michezo nane na kufanikiwa kushinda mchezo mmoja leo imefanikiwa kutoa gundu hilo baada ya kuwafunga Crystal Palace goli moja kwa bila. Goli pekee la klabu hiyo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa klabu hiyo Kai Havertz.
Huu unakua ushindi wa pili katika michezo tisa ambayo klabu hiyo imefanikiwa kucheza siku za hivi karibuni, Huku wakifanikiwa kufikisha alama 28 kwenye ligi kuu ya Uingereza lakini wameshindwa kupiga hatua kwenye nafasi baada ya kusalia katika nafasi ya 10.
Klabu ya Chelsea leo imeweza kushinda mchezo wake wa pili kati ya michezo mitano ya ligi kuu ya Uingereza waliyocheza baada ya michuano ya kombe la dunia, Lakini Vilevile unakua ushindi wao wa nane katika michezo 19 waliyocheza msimu huu.
Chelsea pia wamefanikiwa kumtambulisha mchezaji wao mpya waliomsajili kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine Mykhaylo Mudryk. Hivo mchezaji huyo ni rasmi ni mali ya The Blues kwasasa baada ya kufatiliwa na klabu ya Arsenal kwa muda mrefu.

