Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo katika Dimba la Mkapa pale Yanga watawaalika Ihefu FC kusaka pointi 3 ambazo walizipoteza mchezo waliokutana mara ya kwanza.

Yanga ilipoteza mechi yake ya kwanza msimu huu kwa Ihefu kwa kuchapwa mabao 2-1 mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika na hawakuamini kilichokuwa kinatokea kwani kipindi hicho timu hiyo ilikuwa inashikilia mkia.
Leo hii wanakutana tena huku vijana wa Nabi wakiwakosa baadhi ya wachezaji wao akiwepo Aziz Ki, Bangala na Bernad Morrison lakini nahodha wa klabu yao Mwamnyeto amesema pointi tatu ni muhimu.

Wakiwa kileleni na pointi zao 50 baada ya kucheza mechi 19 wanataka pia kutetea taji hili kwa mara ya pili mfululizo, lakini vijana kutoka Mbarali nao wanahitaji alama kuweza kutoka katika nafasi ya 13 waliyopo kwani sio nzuri.
Mchezo huo utapigwa kmajira ya saa 12:30 jioni ambapo tiketi zilishatoka mapema na viingilio vilishatajwa.

