Klabu ya Yanga imelamba tena Milioni 10 za mama Samia hapo jana baada ya kuikandamiza Real Bamako mabao 2-0 katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Mabao hayo ya ushindi yalitupiwa kimyani na mshambuliaji Fiston Mayele katika dakika ya 08 ya mchezo pamoja na Jesus Moloko katika dakika ya 68 ya mchezo huku Bamako wao mambo yakizidi kuwaendea kombo.
Baada ya ushindi huo wa jana Yanga wapo nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi zao 07, huku kinara wa kundi hilo akiwa ni US Monastir ambaye alishinda pia jana na kufikisha pointi 10.

Mechi inayofuata atamenyana dhidi ya US Monastir huku mechi ya mwanzo walipokutana vijana wa Nabi walipoteza wakiwa ugenini. Baada ya kupoteza mechi ya jana Bamako wanazidi kushikilia mkia.

