Guardiola:Ushindi dhidi ya Liverpool ni Ushindi bora zaidi Kwangu

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amewapongeza wachezaji wake kutokana na kiwango walichokionesha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool na kufanikiwa kupata alama tatu na kusema ni ushindi bora zaidi kwake.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Etihad ukishuhudia Manchester City wakigawa kipigo kizito kwa Liverpool cha mabao 4-1, Kitu kilichomfanya kuamini namna wamecheza katika mchezo huo basi ushindi huu unakua moja ya ushindi wake bora kabisa katika ukocha.GuardiolaKocha huyo anaamini wachezaji wake walicheza vizuri kuanzia dakika ya kwanza hadi dakika 93, Hata pale walipotanguliwa kwa bao moja na Liverpool lakini wao waliendelea kucheza vizuri na ndio sababu iliyowafanya kupata matokeo ya ushindi, Kocha anasema Liverpool nao walikua tishio zaidi hasa walipokua wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kocha Guardiola amemsifu mshambuliaji wake kinda wa kimatifa wa Argentina Julian Alvarez ambae amechukua nafasi ya Earling Haaland ambaye alipata majeraha na kushindwa kucheza mchezo katika mchezo huo, Lakini Alvarez alicheza vizuri na kumkosha kocha wake.GuardiolaGuardiola pia amempakulia minyama mchzaji wake ghali klabuni hapo ambaye amekua akitupiwa lawama mara kwa mara kwa kudaiwa anacheza chini ya kiwango Jack Grealish, Lakini leo amecheza mchezo mzuri sana dhidi ya Liverpool na kocha wake kusema huyu ndo Grealish ambaye tulimjua.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.