Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay Federico Valverde ameripotiwa kumpiga mchezaji wa klabu ya Villarreal baada ya mchezo uliozikutanisha timu hizo katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kiungo wa Valverde inaelezwa alimshambulia mchezaji wa klabu ya Villarreal Alex Baena baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Taarifa zinaeleza kiungo huyo alimpiga mchezaji huyo wa Villarreal baada ya kumsubiri kwenye sehemu ya magari yanapoegeshwa na kumshambulia.
Ugomvi baina ya kiungo huyo wa klabu ya Real Madrid na mchezaji Alex Baena wa Villarreal unaelezwa ulianzia uwanjani ambapo mchezaji Baena alimtolea maneno machafu kiungo Federico ya kua anapaswa kulia kwasababu mwanaye hatazaliwa tena jambo lililomkasirisha kiungo huyo.
Mwezi Febuari mwaka huu inaelzwa kiungo Valverde alipitia changamoto yeye na mpenzi wake kwani mpenzi wake anaefahamika kama Mina Bonino aliekua mjamzito lakini ujauzito uliharibika, Hivo kitendo cha Baena kutoa kauli ya kejeli kwa kiungo huyo ilieipotiwa kumkera zaidi fundi huyo na kuamua kumshambulia Baena.
Taarifa za Valverde kumshambulia Baena baada ya mchezo wa jana kati ya Real Madrid dhidi ya Villarreal limethibitishwa ni la kweli, Lakini uchunguzi bado unaendelea kufanyika zaidi na mamlaka ili kujua chanzo halisi cha ugomvi huo ili hatua zingine za kisheria ziweze kufuatwa.

