Newcastle Yafanya Mauaji Yaipiga Spurs Sita

Klabu ya Newcastle United imefanya mauaji makubwa katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo waliikaribisha klabu ya Tottenham Hotspurs na kuibamiza kwa mabao sita kwa moja.

Newcastle walianza mchezo huo kwa kasi baada ya kufanikiwa kupata bao dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Jacob Murphy, Huku wakiendelea kufanya mashambulizi makali kuelekea lango la Spurs na mpaka kufikia dakika ya 9 ya mchezo vijana wa Eddie Howe walikua mbele kwa mabao matatu yaliyofungwa na Murphy na Joelington.NewcastleKlabu ya Tottenham ilionekana kupoteana zaidi ndani ya dakika 15 za awali na kuwafanya vijana wa Eddie Howe kupata mabao matatu mpaka dakika hizo, Mpaka kufikia mapumziko mshambuliaji Alexender Isak aliongeza mabao mawili na kufanya Spurs kua nyuma kwa mabao matano kwa bila mapumziko.

 

Newcastle walirejea kipindi cha pili kwa kasi kama walivyoanza kipindi cha kwanza na kuendelea kutengeneza nafasi zaidi, Lakini ni Spurs waliopata goli la kufutia machozi dakika ya 49 ya mchezo kupitia kwa Harry Kane lakini haikiwaondoa Magpies mchezoni kwani waliweza kuweka bao la sitta kambani kupitia kwa Callum Wilson na kuhitimisha karamu ya mabao kwa timu hiyo.NewcastleKlabu ya Newcastle United sasa watakua wamewaacha nyuma Tottenham kwa alama sita baada ya kufikisha alama 59 huku Spurs wakibaki na alama 53, Hii inaonesha ni kama taratibu Tottenham wanaaga mbio za kuwania nafasi nne za juu kwa msimu huu kwani klabu ya Manchester United ambayo ipo nafasi ya nne imeacha Spurs kwa alama sita huku Man United wakiwa na viporo vya mechi mbili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.