Beki wa klabu ya Everton raia wa kimataifa wa Uingereza James Tarkowski ndio mchezaji wa ndani aliefanikiwa kucheza dakika zote kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza msimu wa mwaka 2022/23.
James Tarkowski amefanikiwa kucheza dakika zote kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu akfanikiwa kucheza dakika zote 90 kwenye michezo 38 ya ligi hiyo msimu huu, Beki huyo amefanikiwa kucheza dakika 3420 ambazo zimemuweka kileleni kwa wachezaji wa ndani kwenye ligi hiyo msimu huu.
Mbali na beki huyo kufanikiwa kucheza dakika hizo kama mchezaji wa ndani lakini vilevile magolikipa ambao sio wachezaji wa ndani nao wamefanikiwa magolikipa wawili ambao ni Aaron Ramsdale, David de Gea nao wamefanikiwa kucheza dakika 3420 ndani ya msimu huu na wao kua magolikipa waliofanikiwa kucheza dakika zote msimu huu.
Beki James Tarkowski amekua moja ya nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Everton kwani amefanikiwa kucheza kwa kiwango cha juu msimu ndani ya timu hiyo, Akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza tangu kwa kocha Frank Lampard mpaka kocha Sean Dyche nae pia alimuamini.
James Tarkowski ambaye alijiunga klabu hiyo kutoka Burnley msimu uliomalizika amekua na msimu bora sana ndani ya Everton, Huku akiwa moja ya wachezaji waliochangia klabu hiyo iweze kubakia ndani ya ligi ya Uingereza kutokana na uwezo mkubwa ambao amekua akiuonesha kwenye michezo ya timu hiyo.

