Mshambuliaji wa klabu ya Eintracht Frankfurt na timu ya taifa ya Ufaransa Kolo Muani amekaribia kujiunga na mabingwa ligi kuu ya Ufaransa klabu ya PSG baada ya kufikia makubaliano.
Kolo Muani amekubaliana na klabu ya PSG maslahi binafsi pamoja na mkataba wa miaka mitano, Huku ikiwa inasubiriwa klabu ya Frankfurt kupokea ofa kutoka PSG na kumuuza mchezaji huyo.
Mabingwa wa soka Ufaransa wanafanya usajili wa nguvu katika kuhakikisha wanaifanya klabu hiyo kua tishio zaidi msimu ujao,Kwani mpaka sasa wameshafanya sajili kadhaa ambazo zinaonesha wamepania kua bora.
Klabu ya PSG chini ya kocha Luis Enrique tayari wameshafanikiwa kumsajili mshambuliaji Goncalo Ramos, Ousmane Dembele, Manuel Ugarte lakini pia wamefanikiwa kumbakiza mshambuliaji wake matata klabuni hapo Kylian Mbappe.
Mshambuliaji Kolo Muani nae yuko njiani kujiunga na klabu ya PSG ikiwa atakwenda kuunda safu hatari ya ushambuliaji ndani ya klabu hiyo, Hiyo ni kutokana na ubora wake ambao amekua akiuonesha kwenye klabu yake ya Frankfurt ya nchini Ujerumani.

