Valencia Amsifia Garnacho

Winga na nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United Antonio Valencia amemsifia kinda wa klabu hiyo Alejandro Garnacho kutokana na ubora ambao anaouonesha klabuni hapo.

Valencia anasema anamuona Garnacho anaimarika siku baada ya siku huku akimuona akiweza kufanya makubwa zaidi siku za usoni, Hii inanaonesha ni namna gani watu wameeka matumaini kwa kinda Garnacho.valenciaKinda Garnacho ambaye alipata muda wa kucheza zaidi kwenye kikosi cha Manchester United msimu uliomalizika, Hii imefanya watu wengi kuamini mchezaji huyo atakuja kufanya makubwa katika kikosi cha Man United kama ataendelea kuonesha ubora.

Mkongwe Valencia anaamini mashabiki wa Manchester United wanatamani kumuona Garnacho anacheza kwasababu ya uwezo ambao amekua akiuonesha na wanaamini anastahili kupata nafasi hiyo.valenciaWinga Alejandro Garnacho amekua akiaminiwa na kocha Erik Ten Hag licha ya umri wake mdogo, Hii inakumbusha mashabiki wa Man United kipindi cha gwiji Cristiano Ronaldo alipoaminiwa kwenye umri mdogo na Sir Alex Ferguson na akafanikiwa kufanya makubwa klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.