Mama wa beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Harry Maguire ameonesha kusikitishwa na kinachoendelea juu ya mwanao siku za hivi karibuni.
Mama yake Maguire kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amelaani vitendo vinavyoendelea dhidi ya mwanae kwani amesema mashabiki wanachokifanya kwasasa juu ya beki huyo ni zaidi ya kawaida.
Mama wa beki huyo ameeleza “Ninatambua kwenye mpira wa miguu kuna kupanda na kushuka lakini ambacho Harry anakipokea ni zaidi ya mpira wa miguu” Alisema Mama wa beki huyo kwa masikitiko makubwa.
Mama huyo ameeleza anachukizwa na anachokipitia beki huyo na yeye kama Mzazi hatapenda kuona mtu mwingine akipitia ambacho anapitia, Huku akimsifu beki huyo kwa kusema ana moyo mgumu lakini pia ana nguvu kiakili kwani alichoweza kuvumilia yeye wengine wameshindwa.
Beki Harry Maguire amekua akipokea ukosoaji unaoambatana na kejeli na matusi kutokana na kushuka kwa ubora wake, Jmabo ambalo limemfanya Mama yake mzazi kutoka hadharani na kukemea ambacho kinaendelea juu ya mwanae.

