Mama Yake Maguire Asikitishwa na Ubaguzi wa Mwanae

Mama wa beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Harry Maguire ameonesha kusikitishwa na kinachoendelea juu ya mwanao siku za hivi karibuni.

Mama yake Maguire kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amelaani vitendo vinavyoendelea dhidi ya mwanae kwani amesema mashabiki wanachokifanya kwasasa juu ya beki huyo ni zaidi ya kawaida.MaguireMama wa beki huyo ameeleza “Ninatambua kwenye mpira wa miguu kuna kupanda na kushuka lakini ambacho Harry anakipokea ni zaidi ya mpira wa miguu” Alisema Mama wa beki huyo kwa masikitiko makubwa.

Mama huyo ameeleza anachukizwa na anachokipitia beki huyo na yeye kama Mzazi hatapenda kuona mtu mwingine akipitia ambacho anapitia, Huku akimsifu beki huyo kwa kusema ana moyo mgumu lakini pia ana nguvu kiakili kwani alichoweza kuvumilia yeye wengine wameshindwa.MaguireBeki Harry Maguire amekua akipokea ukosoaji unaoambatana na kejeli na matusi kutokana na kushuka kwa ubora wake, Jmabo ambalo limemfanya Mama yake mzazi kutoka hadharani na kukemea ambacho kinaendelea juu ya mwanae.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.