Aston Villa Kuibomoa Chelsea
Makala iliyopita
Ratcliffe: Tunataka kua kama Real Madrid
Makala ijayo
PSG Wamvizia Fundi Rayan Cherki
Chelsea wanatarajia kupokea kiasi cha £37.5 milioni kutoka klabu ya Villa kama ada ya uhamisho wa beki Ian Maatsen ambaye amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Borussia Dortmund huku akiwa sehemu ya wachezaji muhimu ndani ya Dortmund waliopambana kuipeleka Dortmund fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.
Mpaka sasa klabu ya Aston Villa imeshamalizana na beki Ian Maatsen katika suala maslahi binafsi kinachosubiriwa ni klabu ya Chelsea kupokea ada ya uhamisho kutoka kwa Villa ili dili hilo likamilike, Klabu ya Aston Villa wanaelezwa wanahitaji kukamilisha dili hilo kabla ya michuano ya Euro kumalizika.