Klabu ya PSG inamfukuzia kiungo fundi wa klabu ya Olympique Lyon raia wa kimataifa wa Ufaransa Rayan Cherki ambaye amekua moja ya wachezaji wanaomvutia kocha Luis Enrique.
Kocha wa klabu ya PSG Luis Enrique inaelezwa ni shabiki mkubwa wa kiungo Rayan Cherki na anamuhitaji aje aongeze nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao wa mwaka 2024/25 ambao klabu hiyo ina mipango mikubwa haswa kwenye ligi ya mabingwa ulaya.
Kiungo Rayan Cherki amekua akifukuziwa na vilabu vingine barani ulaya kama klabu ya Chelsea ambayo ilikua inahitaji saini yake dirisha kubwa lililopita, Lakini kwasasa klabu ya PSG mabingwa wa Ufaransa wanaonekana wako kwenye mbio wenyewe hivo inaweza kua rahisa kumpata kiungo huyo.
Klabu ya PSG chini ya kocha Luis Enrique inahitaji kutengeneza timu mpya iliyoundwa na vijana wadogo wenye ubora mkubwa ili kuweza kutimiza ndoto za matajiri wa klabu hiyo ambao wana ndoto ya kuona klabu hiyo inatwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya siku moja.