PSG Yamuwinda Joao Neves

Klabu ya PSG mabingwa wa soka nchini Ufaransa nao wameingia kwenye mbio za kumuwinda kiungo wa klabu ya Benfica raia wa kimataifa wa Ureno Joao Neves ambaye anawinda na vilabu kadhaa barani ulaya.

PSG wanamuhitaji kiungo Joao Neves kwajili ya kuimarisha safu yao ya ulinzi kuelekea msimu ujao chini ya kocha Luis Enrique ambaye ameaminiwa klabuni hapo, Bei ya kiungo huyo ndio imekua changamoto mpaka sasa vilabu vingine vikiendelea kujiuliza kama wanaweza kutoa kiasi hicho cha pesa.PSGKlabu ya Benfica inasema haimuachii kiungo huyo chini ya ada ya uhamisho ya €120 milioni jambo ambalo limewafanya vilabu vingine kama Arsenal na Man United ambao wamekua wakimfukuzia kutulia kwanza, Klabu ya Benfica miaka ya hivi karibuni wamekua wakifanya biashara yenye faida kubwa sana wakiuza wachezaji chini ya Rais wa klabu hiyo Manuel Rui Costa.

Joao Neves amekua kwenye kiwango kikubwa sana na amefanikiwa kua mchezaji tegemezi ndani ya kikosi cha Benfica licha ya umri wake mdogo wa miaka (19) na mpaka kufikia kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambacho kinashiriki michuano ya Euro mwezi huu pale nchini Ujerumani.PSGMpaka sasa inaonekana mwenye kisu kikali ndio atakula nyama kwa maana ya kwamba klabu ambayo itatoa dau nono ambalo wanataka klabu ya Benfica ndio watapata saini ya kiungo huyo, Kwani vilabu kama Man United, Arsenal, PSG ambao waingia kwenye mbio hivi karibuni wanaitaka saini ya kiungo huyo mwenye ubora mkubwa.

Acha ujumbe