Mchezaji wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uturuki Nuri Sahin ametangazwa rasmi kurithi mikoba ya aliyekua kocha wa timu Dortmund Edin Terzic.
Kocha Edin Terzic alitangaza kuachana na klabu ya Borussia Dortmund siku ya jana baada ya kudumu ndani ya klabu kwa takribani miaka 10 kama mtumishi wa timu hiyo, Hivo kiungo Nri Sahin ametangazwa kuchukua mikoba ya kocha huyo kuanzia msimu ujao.Kiungo huyo ambaye msimu ulimalizika alikua kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo naye amefata nyendo za Edin Terzic ambaye alikua sehemu ya benchi la ufundi la klabu hiyo kabla ya kukabidhidwa majukumu mazito ya kuiongoza klabu ya Borussia Dortmund kwa misimu miwili na nusu.
Kinachosubiriwa ni kuona Nuri Sahin akifanya makubwa ndani ya klabu hiyo kama ambavyo mtangulizi wake Edin Terzic alifanya ambapo alifanikiwa kushinda taji la DFB Pokal, pamoja na kuifikisha klabu hiyo hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kupita miaka 10.Nuri Sahin amefanikiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu ujao kama kocha mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund, Lakini mkataba huo haujawekwa wazi kua amesaini mkataba wa miaka mingapi ndani ya timu hiyo jambo ambalo linaweza kuwekwa wazi katika siku zinazofuata.