Marco Reus Mfalme wa Signal Iduna Park na Tegemeo la Dortmund

Marco Reus ni mfalme pale Signal Iduna Park , akilala akiamka bado ni mfalme watu wanakwenda wanapita wanamuacha pale . Ni kama mapenzi vile yaani kumvumilia mwenza wako katika hali yoyote , wengine wanasema mapenzi ya kweli yaliisha miaka ya 80 hakuna mapenzi saivi zaidi ya kusaidiana tu , hakuna mapenzi ya Agape saivi kila mtu anawaza faida yake . Penzi la Marco Reus na Borrusia Dortmund ni la Agape kila mtu anampenda mwenzake.

Marco Reus

Marco Reus alianza katika timu za watoto za Borrusia Dortmund kabla ya kutimka kutafuta uzoefu Rot Weiss ahlen II na Borussia Monchengladbach aliwasha moto mkubwa na Dortmund kuamua kumrudisha nyumbani Signal Iduna Park . Mashabiki wa Borrusia wameweza kumpenda na wameshindwa kumchukia , amewaingia kwenye nyoyo zao na anawakosha , wakati Piere Aubemeyang anawaletea nyodo anataka kuhama wala hawakua na presha walijua Reus akitoka kitandani basi anakua boss . Mashikaji wake Roberto Lewandowski aliondoka yeye akabaki , aliondoka Shinji Kagawa , Mario Gotze , Nuri Sahin , Aubemeyang na mafundi wengine kibao lakini yeye hana huo muda , akitoka majeruhi wanamrudishia tambala la unahodha.

Miasha yake yametawaliwa na majeraha sio kila timu inauwezo wa kua na Marco Reus , Kizuri kwake akipona hahitaji muda mwingi kurudisha form yake anakupa kitu kizuri ambacho wachezaji timamu hawakupi . Muunganiko wake na Mario Gotze pale Dortmund enzi za Klopp ulisemekana ni hatari zaidii kwa kipindi kile. Kuelekea kombe la dunia 2014 pale Brazill alicheza mechi sita alifunga goli tano na assists tatu , ilibidi aondolewe katika timu itakayoshiriki kombe la dunia baada ya kuumia katika mechi ya kirafiki dhidi Armenia alilia sanaa..

Marco Reus

Mashabiki wengi wa mpira waliaimini na wanaamini Reus hakutakiwa kuendelea kukaa pale Dortmund , katika ubora wake huwezi kumkataa kukaa kwake Bundersliga tena Dortmund sawa na kuishi gizani nani atamuona na kumzingatia ?? pengine ni bora ambavyo hakuondoka sababu hakuna uhakika wa moja kwa moja kwamba atang’aa pamoja na majeraha yake . Marco Reus ni kiungo mshambuliaji mwenye kasi kubwaa , uwezo wa kumilikia mpira ,uwezo mkubwa wa kufunga , anapiga kwa uzuri mpira iliyokufa na kikubwa anapiga mashuti makali mnooo.

Ameamua kuwatumikia BVB milele daima , hana dalili za kuondoka na inawezekana hafikirii , ameona kuna ufalme wake pale pamoja na swahiba wake Mario Gotze watoto wa kishua hawa . Wazazi wake waliamua kumpa jina la Marco ili kumuenzi legend wa soka wa Uholanzi Marco Van Basten , Reus ataendelea kua moja ya wachezaji bora kabisa katika kizazi chake alikua namba tatu katika wachezaji bora duniani mwaka 2013.

34 Komentara

    Marco Reus ni kiungo mshambuliaji mwenye kasi kubwaa ssna

    Jibu

    Asante meridianbet kwa makala ya uwakika.

    Jibu

    Marco reus yuko vizuri

    Jibu

    Reus ni mchezaji mwenye kijapi cha hali ya juu na ameisaidia sana Dortmund

    Jibu

    Ni mchezaji mzur

    Jibu

    Reus yupo vzr Sana ana nidhamu kubwa

    Jibu

    huyu reus atazeekea hapo

    Jibu

    Nikiungo mpambanaji sana na ndio mana dortmund inamtegemea sana

    Jibu

    Nakala nzuri #meridianbettz

    Jibu

    Kiungo mzuri mwenye nidhamu& kujituma

    Jibu

    Nimchezaji mzuri sanaaa

    Jibu

    Reus yuko vzr mno

    Jibu

    ameona kuna ufalme wake pale pamoja na swahiba wake Mario Gotze watoto wa kishua hawa

    Jibu

    Hajakosea kwa hilo Reus yuko sawa kabisa

    Jibu

    Nimchezaji maridadi

    Jibu

    Namkubal sana

    Jibu

    Marco reus Yuko vizuri

    Jibu

    Reus ni mfalme watu wanakwenda wanapita wanamucha

    Jibu

    Mchezaji Yuko vizur

    Jibu

    duuh huyo bwana mdogo atazeekea hapo#meridianbettz

    Jibu

    Reus Ana kipaji na anajua mpira sanaa

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri pia Ni mpambanaji

    Jibu

    Mashabiki wa Borrusia wameweza kumpenda na wameshindwa kumchukia marco lous

    Jibu

    Reus amenikumbusha mapenzi aliyonayo Ramos kwa Real Madrid#meridianbettz

    Jibu

    marco reus yuko poa sana

    Jibu

    Huyo n kiungo mzur sana Dortmund

    Jibu

    Reus yupo vizuri..

    Jibu

    Namkubar Sana Reus

    Jibu

    Reus yupo vizuri sana

    Jibu

    Kiungo hatar huyo

    Jibu

    Mchezaji mzur sana huyo

    Jibu

    Talent player

    Jibu

    Reus ni mchezaji mwenye kipaji Cha pekee na anatambua alifanyalo

    Jibu

    Mchezaji mzur

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.