Manchester United Yamvalia Njuga Zirkzee

Makala iliyopita
PSG Wamvizia Fundi Rayan CherkiMakala ijayo
Serbia Ngoma Hali Tete Euro 2024
Klabu ya Ac Milan inaelezwa ilikua karibu zaidi kumsajili mshambuliaji Joshua Zirkzee kutoka Bologna na maslahi binafsi baina ya pande hizo yalishakubaliwa, Lakini Man United wanaonekana kama wanaweza kupindua meza kwakua wako tayari kutoa kiasi husika kinachohitajika.
Sehemu nyingine ambayo klabu ya Manchester United wameonekana kuipiga bao mpaka sasa Ac Milan ni kwa wakala wa mshambuliaji huyo, Ambapo Man United wamekubali kulipa kamisheni ya mauzo ya mchezaji kwa wakala huyo jambo ambalo litarahisisha Mashetani wekundu kumpata mchezaji huyo.