Aston Villa Kuibomoa Chelsea

Klabu ya Aston Villa ipo mbioni kumalizana na beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Uholanzi ambaye alikua anakipiga kwa mkopo klabu ya Borussia Dortmund Ian Maatsen.

Aston Villa chini ya kocha Unai Emery ambapo msimu ujao watacheza ligi ya mabingwa ulaya hivo wanahitaji kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao, Hivo beki Ian Maatsen amekua pendekezo la kwanza kwa klabu hiyo katika maboresho kuelekea msimu ujao.aston villaChelsea wanatarajia kupokea kiasi cha £37.5 milioni kutoka klabu ya Villa kama ada ya uhamisho wa beki Ian Maatsen ambaye amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Borussia Dortmund huku akiwa sehemu ya wachezaji muhimu ndani ya Dortmund waliopambana kuipeleka Dortmund fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.

Klabu ya Borussia Dortmund mwanzo walionekana wangeweza kumsajili mchezaji huyo kwa uhamisho wa kudumu baada ya kuonesha kiwango bora ndani ya timu hiyo, Kwani klabu ya Chelsea ilishaonesha nia ya kumuuza mchezaji huyo lakini Villa wamefanikiwa kuipiku klabu hiyo na wako kwenye hatua za mwishoni kukamilisha dili hilo.aston villaMpaka sasa klabu ya Aston Villa imeshamalizana na beki Ian Maatsen katika suala maslahi binafsi kinachosubiriwa ni klabu ya Chelsea kupokea ada ya uhamisho kutoka kwa Villa ili dili hilo likamilike, Klabu ya Aston Villa wanaelezwa wanahitaji kukamilisha dili hilo kabla ya michuano ya Euro kumalizika.

Acha ujumbe