Klabu ya West Ham inaelezwa imekubaliana na beki wa kulia wa klabu ya Manchester United Aaron Wan Bissaka kwajili ya kujiunga na klabu hiyo msimu ujao.
Klabu ya West Ham inaelezwa imetuma kiasi cha paundi milioni 10 kwa klabu ya Manchester United lakini klabu hiyo inahitaji kiasi cha paundi milioni 18 ili kumuachia beki huyo ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka mitano sasa, Hivo hii inaweza kua changamoto kwa klabu hiyo kutoka jiji la London.