West Ham Wamalizana na Wan Bissaka

Klabu ya West Ham inaelezwa imekubaliana na beki wa kulia wa klabu ya Manchester United Aaron Wan Bissaka kwajili ya kujiunga na klabu hiyo msimu ujao.

 

Wan Bissaka yupo tayari kuondoka ndani ya viunga vya Old Trafford na kujiunga na West Ham baada ya klabu hiyo kutimiza vigezo ambavyo mchezaji huyo amevihitaji, Lakini bado wagonga nyundo hao kutoka jiji la London wana mtihani wa kuishawishi klabu ya Man United kumuachia mchezaji huyo.west hamKlabu ya West Ham inaelezwa imetuma kiasi cha paundi milioni 10 kwa klabu ya Manchester United lakini klabu hiyo inahitaji kiasi cha paundi milioni 18 ili kumuachia beki huyo ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka mitano sasa, Hivo hii inaweza kua changamoto kwa klabu hiyo kutoka jiji la London.

Manchester United wako tayari kumuuza Wan Bissaka lakini endapo tu klabu inayomuhitaji mchezaji huyo itafikia dau ambalo wamelihitaji, Hivo klabu ya West Ham inatakiwa kufikia dau ambalo Man United walihitaji kwani kumalizana na mchezaji pekee haitoshi lazima pia wafikie dau ambalo klabu miliki ya mchezaji imehitaji.

Acha ujumbe