Borussia Dortmund Waiwekea Ngumu Juventus kwa Adeyemi

Klabu ya Borussia Dortmund imewawekea ngumu klabu ya Juventus ambao walikua wanamfukuzia kwa karibu winga wa klabu yao Karim Adeyemi raia wa kimataifa wa Ujerumani.

Juventus walielezwa kuwasiliana na winga Karim Adeyemi na winga huyo alionekana kushawishika na mkakati wa muda mrefu ambao klabu hiyo inao, Lakini Borussia Dortmund wanaelezwa kusitisha mpango wa kumuuza winga Adeyemi na mkakati wao kwasasa ni kubaki na mchezaji huyo.borussia dortmundTaarifa zinaeleza kua klabu ya Juventus hawakuwahi kutuma ofa yeyote rasmi kwa Dortmund na mazungumzo yalikua baina yao na upande wa mchezaji tu, Huku wanafainali hao wa ligi ya mabingwa ulaya wakiona kama winga Karim Adeyemi ni moja ya wachezaji wao muhimu kwa miaka kadhaa mbele.

Karim Adeyemi amekua moja ya washambuliaji wenye uwezo mkubwa ndani ya kikosi cha Borussia Dortmund jambo ambalo liliwafanya klabu ya Juventus kuitaka saini ya winga huyo mwenye umri wa miaka (22), Miamba hiyo ya soka kutoka nchini Uingereza wamegoma na wana mpango wa kubaki na winga huyo kwa muda mrefu zaidi.

Acha ujumbe