Stars Kukipiga Na Bafana Bafana Usiku Wa Leo

Timu ya taifa ya Tanzania inataraji kuingia dimbani usiku wa leo kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Bafana bafana ya Afrika kusini, unaotaraji kuchezwa kwenye uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane.

Stars Kukipiga Na Bafana Bafana usiku wa Leo

Mchezo huo utapigwa mnamo saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika mashariki, na mchezo huo japo ni wa kirafiki lakini unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na aina ya wachezaji walioitwa kwenye vikosi vyote, lakini pia mchezo huu unatumika kwa ajili ya maandalizi kuelekea michuano ya COSAFA.

Stars wanautumia mchezo huu kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao ya kundi C ya COSAFA dhidi ya Eswatin na Madagascar. Akizungumza, Kocha mkuu, Hemed Suleiman Morocco amesema kwamba mchezo huu utakua sehemu muhimu ya yeye kutathmini ubora na uimara wa kikosi chake kuelekea michezo hiyo muhimu.

 

Stars Kukipiga Na Bafana Bafana usiku wa Leo

Kocha huyo pia alieleza kuwa mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya mpango mpana wa maandalizi kuelekea Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayofanyika Agosti 2025, pamoja na kurejea kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi Septemba.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Mara ya mwisho Taifa Stars ilicheza mwezi Machi ambapo ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Morocco kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia, kundi E. Hivyo, mchezo wa leo utakuwa kipimo kingine cha maendeleo ya kikosi hicho tangu kipindi hicho.

Kikosi cha Stars kina mchanganyiko wa wachezaji wa ligi ya nyumbani na wale wanaocheza nje ya nchi, wakiwemo nyota wa Simba SC ambao walifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Wachezaji wa kimataifa walioteuliwa katika kikosi hicho ni pamoja na Simon Msuva (Al Talaba, Iraq), Selemani Mwalimu (Wydad AC, Morocco), na Alphonce Mabula (Shamakhi, Azerbaijan), ambao wote wanatarajiwa kuleta uzoefu na ubora wa kiwango cha kimataifa.

Stars Kukipiga Na Bafana Bafana usiku wa Leo

Kwa upande wa historia ya mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini, timu hizo zimekutana mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2002 katika mashindano ya Four Nations ambapo walitoka sare ya 1-1, kisha Taifa Stars kushinda kwa mikwaju ya penalti. Mwaka 2011 Afrika Kusini ilishinda 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki, kabla ya Tanzania kuibuka na ushindi wa 1-0 katika michuano ya COSAFA mwaka 2017.

Kwa kuzingatia maandalizi ya sasa na motisha ya wachezaji, mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya kiwango cha juu na ushindani wa kweli kutoka kwa Taifa Stars.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.