Ureno imetwaa taji la UEFA Nations League kwa mara ya pili baada ya kuifunga Hispania kwa mikwaju ya penalti 5–3, kufuatia sare ya mabao 2–2 ndani ya dakika 120.

Hispania ilianza kwa kasi na kutawala mchezo kupitia pasi fupi za haraka ambazo zilisumbua safu ya ulinzi ya Ureno. Kasi ya Hispania iliwapatia bao la kuongoza dakika ya 21 baada ya Joao Neves kuucheza vibaya mpira wa krosi uliopigwa langoni kwao na Nico Williams. Neves aliupiga mpira hovyo na kumkuta Martin Zubimendi, anayetarajiwa kujiunga na Arsenal, ambaye alifunga kwa urahisi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ureno hawakukata tamaa, na walijibu mapigo dakika tano baadaye. Cristiano Ronaldo alicheza kwa ustadi, akamuwezesha Pedro Neto kutafuta nafasi. Neto alimwona Nuno Mendes pembezoni mwa boksi, na beki huyo wa PSG alikwamisha mpira wavuni kwa shuti la chini lililojaa katika kona ya kulia. Hata hivyo, kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, Hispania walirejea mbele kupitia Mikel Oyarzabal, ambaye alitumia uzembe wa Gonçalo Inácio kumalizia pasi murua ya Pedri na kuipatia La Roja bao la pili.
Kipindi cha pili kilianza kwa ushindani mkubwa, na dakika ya 59, Nuno Mendes aliwashinda mabeki wa Hispania, akampita Yamine Lamal na kutengeneza krosi iliyoguswa na mlinzi na kumkuta Ronaldo. Nahodha huyo wa Ureno aliwazidi nguvu mabeki wa Hispania na kuuweka mpira wavuni kwa ustadi, akifanya matokeo kuwa 2–2 na mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo ulikua bado ni 2-2.

Ziliongezwa dakika 30 za ziada na timu zote zilitengeneza nafasi. Nuno Mendes alikaribia kufunga tena baada ya kupenya na kuangushwa, lakini mwamuzi alikataa kutoa penalti licha ya madai makali. Diogo Costa pia alinusurika baada ya kudaka mpira wa hatari uliopigwa na Pedro Porro kutoka mbali, huku Diogo Jota akipoteza nafasi kwa kichwa.
Hatimaye, mikwaju ya penalti ikalazimika kuamua mshindi. Gonçalo Ramos, Vitinha, Bruno Fernandes, na Nuno Mendes waliifungia Ureno penalti zao kwa ustadi. Kipa Diogo Costa aliokoa penalti ya Álvaro Morata, kabla ya Ruben Neves kuifunga penalti ya mwisho kwa ustadi mkubwa katika kona ya kushoto, na kuihakikishia Ureno taji hilo la Nations League.


