Kikao kilichowakutanisha Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na viongozi wa klabu ya Yanga kimetamatika na Makamu wa Rais wa klabu hiyo ametoa neno kilichojiri ndani ya kikao hicho.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji, amesema klabu yao imeshiriki kikao hicho na kuwasilisha msimamo wa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.
Kikao hicho kilianza saa 4:30 na kumalizika saa 6 mchana na kilifanyika kwenye ofisi za bodi hiyo zilizopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kuhusu mustakabali wa mchezo huo dhidi ya Simba, Arafat amesema Yanga haikuwahi kusema kama itacheza mchezo huo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tumemaliza mkutano na tulichofanya ni kuwasilisha msimamo wa klabu kutoka kwa wanachama na mashabiki wetu hilo ndio kubwa,”amesema Arafat.
Yanga wameweka wazi kwenye taarifa rasmi iliyotolewa na kamati ya utendaji kwamba ni kweli walipokea barua ya wito kutoka bodi ya ligi na kwa kutii wito huo walifika mpaka makao makuu ya bodi ya ligi, walishiriki kikao hicho na viongozi wa Bodi na kuwasilisha msimamo wa klabu kuwa hawatashiriki mchezo namba 184 dhidi ya watani Simba Sc Juni 15, 2025 hadi matakwa yao waliyowasilisha Bodi ya Ligi kwa maandishi yatakapotekelezwa.


