Yanga Waitikia Wito wa Bodi ya Ligi.

Kikao kilichowakutanisha Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na viongozi wa klabu ya Yanga kimetamatika na Makamu wa Rais wa klabu hiyo ametoa neno kilichojiri ndani ya kikao hicho.

Yanga Waitikia Wito wa Bodi ya Ligi

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji, amesema klabu yao imeshiriki kikao hicho na kuwasilisha msimamo wa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Kikao hicho kilianza saa 4:30 na kumalizika saa 6 mchana na kilifanyika kwenye ofisi za bodi hiyo zilizopo Ilala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusu mustakabali wa mchezo huo dhidi ya Simba, Arafat amesema Yanga haikuwahi kusema kama itacheza mchezo huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Tumemaliza mkutano na tulichofanya ni kuwasilisha msimamo wa klabu kutoka kwa wanachama na mashabiki wetu hilo ndio kubwa,”amesema Arafat.

Yanga wameweka wazi kwenye taarifa rasmi iliyotolewa na kamati ya utendaji kwamba ni kweli walipokea barua ya wito kutoka bodi ya ligi na kwa kutii wito huo walifika mpaka makao makuu ya bodi ya ligi, walishiriki kikao hicho na viongozi wa Bodi na kuwasilisha msimamo wa klabu kuwa hawatashiriki mchezo namba 184 dhidi ya watani Simba Sc Juni 15, 2025 hadi matakwa yao waliyowasilisha Bodi ya Ligi kwa maandishi yatakapotekelezwa.

Yanga Waitikia Wito wa Bodi ya Ligi

Kwa upande wa tpbl kupitia mkurugenzi mtendaji, Almas Kasongo wamethibitisha uwepo wa kikao hicho na yale yaliyozungumzwa.

“Leo tulikuwa na Kikao kizuri na Yanga, kwenye Kikao chetu wenzetu wamekuja na mambo Manne na sisi kama Bodi tuna wajibu wa kuyapokea na kuyachakata. Matakwa hayo ni pamoja na kuvunjwa kwa Kamati ya uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu (Kamati ya Saa 72), kujiuzulu kwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (CEO) na Katibu wa Shirikisho la Soka (TFF) pamoja na bodi ya Ligi kubadili muundo na iwe chombo huru na sio sehemu ya TFF.

Ameendelea kwa kusema “Itoshe kusema Uongozi wa Bodi tumepokea maazimio yao na haya yote yapo nje ya Uwezo wa Bodi isipokuwa moja tu la kwanza, tumeyapokea haya mengine matatu na tutayawasilisha kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu na kwenye Mkutano Mkuu.” ameyasema hayo Mkuregenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu Almas Kasongo.”

Vilevile, kwa upande mwingine, Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Ndg. Rashid Mijuza amethibitisha kuwa hawajapokea barua rasmi kutoka timu yoyote kuomba kuutumia uwanja huo, ikiwemo mwenyeji wa mchezo namba 184 ambao ni klabu ya Young Africans, ikielezwa kuwa nao pia hawajatuma maombi ya kutaka kuutumia uwanja huo. Hali inayoleta wasiwasi juu ya uwepo wa mchezo huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.