Klabu ya Yanga kupitia afisa habari wake, Ally Kamwe, ametoa msimamo wa klabu hiyo kuelekea michezo mitatu iliyosalia kumaliza Ligi kuu ya NBC.
Akizungumza mbele ya wanahabari, makao makuu ya klabu, Jangwani, Kamwe amesema walipokea wito kutoka bodi ya ligi kuhusu kikao na walihudhuria lakini kikao hicho hakikuhusu maandalizi ya mechi bali kilihusu sintofahamu ya mchezo namba 182 dhidi ya Simba Sc.

“Ni kweli tulipokea barua ya wito Juni 7 na leo tumeshiriki kikao kama tulivyoombwa na bodi ya Ligi kwenye kikao hiki maalum ambacho hakikuwa cha maandalizi ya mechi bali ni kujadili sintofahamu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu,” alisema Ali Kamwe -Meneja Habari na Mawasiliano Yanga SC
Amesema kwamba kwenye kikao hicho pia waliuliza kuhusu ripoti ya uchunguzi uliofanyika kutokuchezwa kwa mchezo wao dhidi ya Simba tarehe 08 Mei, na mtendaji mkuu wa bodi ya ligi aliwapa majibu ambayo hawakuridhika nayo kama klabu hivyo kuitaka bodi ya ligi kuwa na uwazi na kuelezea kwakina ni sababu zipi zilifanya mchezo huo kuhairishwa.
“Kwenye kikao chetu tuliuliza pia kuhusu ripoti ya kilichotokea Machi 8, na CEO wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo akakiri kuwa ripoti wanayo na kuna kiongozi mkubwa wa Serikali alipiga simu kuzuia geti la uwanja lisifunguliwe, lakini hawawezi kumtaja hadharani. Nashangaa hili hajalisema kwenye tuliyoyazungumza leo, tumshauri akiamua kusema aseme yote asibakishe” aliongezea Ali Kamwe.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Na kuhusu makubaliano ya kikao hicho, kama ilivyoelezewa awali na makamu wa Rais wa klabu hiyo, ni kwamba walienda na mapendekezo yao manne, huku matatu wakitaka yatekelezwe haraka ili klabu ikubali kucheza mchezo wao dhidi ya Simba Sc.
“Tumetoa matakwa manne. Matatu yanahusu mchezo namba 184, tunaamini yakifanyiwa kazi hayo matatu kwanza, tutakuwa tayari kucheza mechi hiyo kwa tarehe nyingine itakayopangwa. Na takwa la nne ni la muda mrefu, kuanzia msimu ujao. CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo asiudanganye umma kwa kuchagua kuzungumzia takwa moja tu na kuacha yanayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu” alisema.
“Takwa letu la kwanza na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni na kuutia doa mpira wetu. Ligi yetu ni kubwa sana Afrika na inataka watu makini wenye weledi kuiongoza” aliongezea meneja huyo wa habari na mawasiliano wa Yanga Sc.

Kuonyesha msisitizo wa klabu juu ya matakwa yao, Ali Kamwe alisema endapo matakwa hayo hayatofanyiwa kazi kwa haraka basi Yanga hawatocheza mchezo wao dhidi ya Simba lakini pia timu haitokuja uwanjani kwenye mechi nyingine mbili za ligi kuu zilizosalia wala kushiriki ligi msimu ujao.
“Napenda kuwajuza waandishi wa Habari, yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka, Young Africans SC hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za Ligi zilizobaki na hatutashiri ligi kuu msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote lile.”
Vilevile, kwa upande wa Kombe la shirikisho la CRDB, Yanga wamewataka TFF na wadhamini kulipwa pesa wanayodai ya ubingwa wa msimu uliopita na bila kulipwa fedha hiyo basi hawatocheza mchezo wa fainali iliyopangwa kuchezwa tarehe 28 huko Zanzibar.
“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa hatutacheza mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa Mamlaka za Soka kwa muda mrefu sana, sasa imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia hatuchezi.”


