Baada ya klabu ya Yanga kutangaza kuwa timu yao haitoshiriki katika fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Singida Black Stars msimu huu hadi pale watakapolipwa fedha za zawadi za ubingwa wa msimu uliopita, benki ya CRDB, mdhamini mkuu wa mashindano hayo, imetoa taarifa rasmi kuyakanusha madai hayo.

Katika taarifa yake ya Juni 10, 2025, benki hiyo imesema kuwa imekamilisha malipo yote ya fedha za zawadi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mujibu wa mkataba wao wa udhamini.
“Benki ya CRDB inazingatia viwango vya juu vya weledi na taratibu za kifedha. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanywa kwa TFF kama ilivyokubaliwa. Tunawahimiza wadau wote wa soka kuthibitisha taarifa hizi kupitia TFF,” ilisema taarifa hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa


