Madai Ya Yanga Yawaibua CRDB

Baada ya klabu ya Yanga kutangaza kuwa timu yao haitoshiriki katika fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Singida Black Stars msimu huu hadi pale watakapolipwa fedha za zawadi za ubingwa wa msimu uliopita, benki ya CRDB, mdhamini mkuu wa mashindano hayo, imetoa taarifa rasmi kuyakanusha madai hayo.

Madai Ya Yanga Yawaibua CRDB

Katika taarifa yake ya Juni 10, 2025, benki hiyo imesema kuwa imekamilisha malipo yote ya fedha za zawadi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mujibu wa mkataba wao wa udhamini.

“Benki ya CRDB inazingatia viwango vya juu vya weledi na taratibu za kifedha. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanywa kwa TFF kama ilivyokubaliwa. Tunawahimiza wadau wote wa soka kuthibitisha taarifa hizi kupitia TFF,” ilisema taarifa hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Madai Ya Yanga Yawaibua CRDB

Aidha, benki hiyo imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kusaidia maendeleo ya soka nchini Tanzania, ikionyesha kuwa mchezo huo sio tu wa burudani bali pia chanzo cha ajira kwa vijana wengi. “Tutashirikiana na TFF, vilabu, na wadau wengine ili kuimarisha soka kwa maslahi ya taifa letu,” taarifa hiyo ikaongeza.

CRDB imetoa wito kwa umma na wadau wa soka kuangalia ukweli wa mambo kupitia mifumo rasmi badala ya kufuata taarifa za upande mmoja.

Mapema klabu ya Yanga kupitia Msemaji wao, Ally Kamwe walisema kwamba hawatoshiriki mchezo wa fainali za mwaka huu zilizopangwa kupigwa Zanzibar mnamo tarehe 28 mwezi huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.