Mchezaji mpya wa soka sasa hatambulishwi kwa mkutano wa waandishi wa habari au nafasi ya kupiga picha za haraka kwenye klabu, imegeuka kuwa tukio linalotumiwa kuingiza pesa kwa timu, tukio linalopangwa kwa makini ili kuwavutia mashabiki.

Jambo hili limeshuhudiwa kwa timu kubwa Duniani kama Real Madrid na Barcelona lakini hata kwa vilabu vya hapa nchini ambavyo utumia matamasha maalumu kutambulisha mchezaji mpya aliyesajiliwa, kwa mfano Simba day na Wiki ya Mwananchi.
Lakini chimbuko la hili suala linaturudisha mpaka Julai 5, 1984, wakati Diego Maradona kwa mara ya kwanza alipotambulisha pale Napoli kwenye uwanja wa Stadio San Paolo. Hii ni siku ambayo Dunia ilishuhudia takriban mashabiki 70,000 waliokuwa na furaha kubwa wakijitokeza uwanjani hapo kushuhudia utambulisho wa mchezaji huyo wa soka kutoka nchini Argentina. Hii ilikua mwanzo wa maonyesho ya utambulisho wa wachezaji.
![]()
Maonyesho ya Maradona yaliweka rekodi mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo vilabu vingine vikubwa vilianza kutumia utaratibu huo kutambulisha sajili zao kubwa. Real Madrid, chini ya Rais Florentino Pérez ilichukua wazo hili na kulitumia kama njia ya utambulisho wa nyota wa kimataifa waliowasajili kama Luís Figo (2000), Zinedine Zidane (2001), Ronaldo (2002), na David Beckham (2003).
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Cristiano Ronaldo alipojiunga na Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa rekodi ya dunia ya euro milioni 94, utambulisho wake ulivunja rekodi ya Dunia kwani mashabiki Zaidi ya 80,000 waliijaza Bernabéu ili kumshuhudia gwiji huyo wa soka akitambulishwa kuwa mchezaji rasmi wa klabu hiyo. Utambulisho wa Ronaldo uliambatana na milipuko ya mafataki, video za matangazo ya moja kwa moja. Hafla hiyo ilitangazwa duniani kote, ikivuta mamilioni ya watazamaji na kutoa habari za vyombo vya habari ambazo hazijawahi kushuhudiwa. Mkakati wa Real Madrid kwenye utambulisho huo haukulenga kumkaribisha pekee ila ilikua kuongeza thamani ya klabu kwa kuongeza mauzo ya jezi, mikataba ya udhamini, na jina la klabu.
Barcelona, wapinzani wakuu wa Real Madrid, walifanya tukio la namna hiyo miaka mine baadae walipomtambulisha mchezaji kutoka Brazir, Neymar (2013). Hafla hizi mara nyingi zilihusisha muziki na maonyesho ya burudani za wasanii wakubwa.

Leo, utambulisho wa wachezaji umekuwa sehemu ya kibiashara ya klabu mbalimbali. Vilabu vingi vya Ulaya na Afrika vimeiga mfumo huu, huku vikijitahidi kutengeneza mvuto na utambulisho wao wa kipekee. Paris Saint-Germain mwaka 2017 walimsajili Neymar kwa rekodi ya dunia ya euro milioni 222 na walifanya tukio kubwa sana la kumkaribisha na kumtambulisha ambapo mnara maarufu Zaidi jijini Paris wa Eiffel uliangazwa kwa rangi za PSG na sherehe hiyo ilivutia mamilioni kwenye mitandao ya kijamii. Vivyo hivyo, utambulisho wa Cristiano Ronaldo pale Al-Nassr kwa mwaka 2023, baada ya kujiunga akitoka Manchester United, ulishuhudia maelfu ya mashabiki wakijaza uwanja wa Mrsool Park huko Riyadh.

Kylian Mbappé alipojiunga na Real Madrid mwaka 2024, mitandao ya kijamii ya klabu hiyo zilitembelewa na watu zaidi ya milioni 50 ndani ya saa 24 za kutambulishwa kwa mchezaji huyo huku uwanja wa Bernabeu ukipokea watu Zaidi ya 80,000 waliojitokeza kushuhudia utambulisho wake. Na sasa tunashuhudia utambulisho mwingine mkubwa ukiwa ni wa Trent Alexander Arnold pale Madrid.

