Mangungu Ni Chuma, Ashikilia Kuti Kavu Simba

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu, amesema uongozi wa klabu hiyo unaendelea kutekeleza majukumu yake kama inavyoelekezwa na katiba, huku akisisitiza kuwa tathmini ya viongozi hufanyika pale muda unapofika.

Mangungu amesema kwa sasa wao kama viongozi wako kazini na hawajafikia hatua ya kujitathmini, akieleza kuwa itakapofika muda sahihi ndipo watakapokaa chini na kufanya tathmini ya kina kuhusu nafasi zao ndani ya uongozi wa klabu.

Mangungu Ni Chuma, Ashikilia Kuti Kavu Simba

Kauli hiyo inakuja kufuatia baadhi ya Wanachama na Mashabiki wa Simba kuibua wito wa kumtaka Mwenyekiti huyo kujiuzulu, wakieleza kutoridhishwa na mwenendo wa timu katika mashindano ya kimataifa msimu huu.

Simba imekuwa na matokeo yasiyoridhisha msimu huu, ikiwemo kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, kutoka sare na Mtibwa Sugar, pamoja na kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumzia presha na makelele kutoka kwa baadhi ya wanachama, Mangungu amesema bado anaendelea na majukumu yake ya kiuongozi bila kuyumbishwa, akisisitiza kuwa haogopi presha wala kelele zisizo na msingi.

“Uongozi ni wa muda na tathmini sahihi hufanywa wakati muafaka unapofika. Uongozi wa Simba si wa mtu mmoja, na baada ya muda wetu kufika tutakaa chini kujitathmini kama tunaweza kuendelea kugombea au kukaa pembeni na kuwaachia wengine,” amesema Mangungu.

Mangungu Ni Chuma, Ashikilia Kuti Kavu Simba

Ameongeza kuwa kwa sasa anaendelea kuratibu mipango na mikakati ya maendeleo ya klabu hadi mwisho wa kipindi chao cha uongozi, huku akibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa wachache wanaopinga, bado anaungwa mkono na idadi kubwa ya Wanachama na Mashabiki wa Simba.

“Wapo wengi wanaoniunga mkono, wananipa moyo wa kuendelea kuitumikia Simba na kunishauri mambo yanayopaswa kurekebishwa. Kwa sasa bado tupo kazini na tutaendelea kuwatumikia Wanasimba kwa bidii hadi pale itakapofika mwisho wa muda wetu au mabadiliko mengine kufanyika kwa mujibu wa taratibu za klabu,” amesema.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.