Klabu ya UD Almeria imefanikiwa kuingia katika nafasi za moja kwa moja za kupanda daraja katika Segunda Division baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Cultural Leonesa. Ushindi huo umevutia macho ya wengi hasa baada ya nyota wa Al-Nassr FC, Cristiano Ronaldo, kununua asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo hivi karibuni.

Matokeo hayo yanaendeleza mwenendo mzuri wa Almeria ambao sasa wameshinda mechi tano kati ya sita zilizopita katika ligi. Mafanikio hayo yamewasogeza hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, nafasi ambayo hawajashikilia tangu mwezi Novemba. Baada ya kushuka daraja kutoka La Liga mwaka 2024, klabu hiyo imeanza kuonyesha dalili za kurejea kwa nguvu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Uwekezaji mpya uliofanywa na kundi la wawekezaji kutoka Saudi Arabia mwaka 2025 pamoja na kuingia kwa Ronaldo katika uongozi wa klabu umeonekana kuipa timu motisha mpya. Ingawa kwa sasa yupo Madrid akipona majeraha ya msuli wa paja, Ronaldo aliendelea kufuatilia maendeleo ya timu hiyo na kupitia Instagram aliandika ujumbe mfupi wa pongezi baada ya ushindi huo: “Great win today. We continue.”

Kocha wa timu hiyo, Juan Francesc Ferrer maarufu kama Rubi, alisisitiza kuwa bado mapambano hayajaisha. Alieleza kuwa lengo ni kubaki kwenye nafasi za juu hadi mwisho wa msimu, akionya kuwa bado kuna pointi nyingi zilizobaki kupiganiwa huku wakijaribu kupunguza pengo la pointi nne dhidi ya vinara Racing Santander.

Katika hatua inayofuata ya mbio za kupanda daraja, Almeria wanakabiliwa na ratiba ngumu ya mechi. Watacheza ugenini dhidi ya Real Zaragoza na SD Huesca kabla ya kurejea nyumbani kumenyana na Real Sociedad B, mechi ambazo zinaweza kuamua mwelekeo wa ndoto yao ya kurejea La Liga.

