Yanga Yawasili Arusha kwa Mchezo Dhidi ya TRA, Simba Kuwafuata Pamba Mwanza

Kikosi cha Yanga sc kimewasili salama jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya  NBC dhidi ya TRA united utakaochezwa Jumatano, Machi 18, 2026 katika Uwanja wa Jamhuri Sheikh Amri Abeid, Arusha majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Yanga imewasili Arusha baada ya kumaliza mchezo wa dabi ya Dar es Salaam dhidi ya Azam fc uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Yanga Yawasili Arusha kwa Mchezo Dhidi ya TRA, Simba Kuwafuata Pamba Mwanza

Katika hatua nyingine, mchezo wa ligi kuu uliopangwa kuzikutanisha Simba na TRA united katika Uwanja wa Sheikh Amri abeid, Arusha uliahirishwa na Bodi ya ligi kutokana na hali mbaya ya hewa iliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa 

Kutokana na kuahirishwa kwa mchezo huo, kikosi cha Simba S.C. kinatarajiwa kuondoka Dar es salaam kesho jioni, Machi 17, 2026 kuelekea Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji fc.

Yanga Yawasili Arusha kwa Mchezo Dhidi ya TRA, Simba Kuwafuata Pamba MwanzaMchezo huo kati ya Simba sc. na Pamba Jiji fc unatarajiwa kuchezwa Machi 19, 2026 majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.