Kocha msaidizi wa Tottenham Hotspur, Bruno Saltor, amekiri kuwa timu yake ilishindwa kukabiliana na presha ya mchezo muhimu wa kupambana na kushuka daraja baada ya kufungwa mabao 3-0 na Nottingham Forest Jumapili.
Kipigo hicho kimeiacha Spurs ikiwa na tofauti ya pointi moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja katika Premier League, hali inayoongeza wasiwasi kwa mashabiki na uongozi wa klabu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Saltor alisimamia mkutano na waandishi wa habari kwa niaba ya kocha mkuu Igor Tudor ambaye alikuwa anashughulikia msiba wa kifamilia. Licha ya matokeo mabaya, alisema kulikuwa na dalili chanya katika mechi mbili zilizopita pamoja na kiwango cha kipindi cha kwanza dhidi ya Forest.
Hata hivyo, alikiri kuwa timu ilipoteza mwelekeo kipindi cha pili na kushindwa kuhimili uzito wa mchezo huo muhimu, jambo lililosababisha kuporomoka kwa kiwango na kuruhusu mabao ya haraka.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Saltor alisema “Unaweza kuona wachezaji wanajali na wanajitahidi kwa asilimia 100, lakini kwa sasa haitoshi. Tunahitaji kupunguza makosa kwa sababu tunajua tutaruhusu mabao.”
Aliongeza “Dakika 44 za kwanza zilikuwa nzuri sana, lakini kipindi cha pili hatukuweza kubeba uzito wa mchezo. Kwa sasa, sote tuna lengo moja kupambana hadi mwisho wa msimu na kubaki kwenye ligi kama klabu hii inavyostahili

