TFF Yaufungia Uwanja wa Jamhuri Dodoma Kwa Kukosa Vigezo vya Kikanuni

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, limetangaza kuufungia rasmi Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma kwa matumizi ya michezo ya Ligi kufuatia kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

TFF Yaufungia Uwanja wa Jamhuri Dodoma Kwa Kukosa Vigezo vya KikanuniKwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Machi 22, 2026, TFF imeeleza kuwa miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa yaliyowekwa chini ya Kanuni za Leseni za Klabu, hali inayolazimu kuchukuliwa kwa hatua hiyo ili kulinda ubora na usalama wa mashindano.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kutokana na uamuzi huo, timu zote zinazotumia Uwanja wa Jamhuri kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutafuta viwanja mbadala kwa muda, hadi pale maboresho yatakapofanyika na kukaguliwa upya na TFF.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa kufunguliwa tena kwa uwanja huo kutategemea kukamilika kwa marekebisho ya miundombinu pamoja na kupitishwa rasmi na mamlaka husika ndani ya TFF.

TFF Yaufungia Uwanja wa Jamhuri Dodoma Kwa Kukosa Vigezo vya KikanuniAidha, TFF imezikumbusha klabu zote nchini kuendelea kuzingatia na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili kuendana na matakwa ya kanuni, hatua inayolenga kuimarisha kiwango cha soka la Tanzania pamoja na ushindani wa ligi zake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.